Kikosi cha Yanga kilicho ivuruga Ngaya Leo |
YANGA SC wameanza vizuri mawindo yao ya ubingwa wa Afrika, baada ya
kwachapa wenyeji Ngaya Club de Mde mabao 5-1 jioni ya leo mjini Moroni,
Comoro.
Ushindi huo unamaanisha Yanga watakuwa na shughuli nyepesi tu katika
mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Dar es Salaam, kwani hata
wakifungwa 3-0 watasonga mbele.
Kiungo Mzambia, Justin Zulu alifungua akaunti yake ya mabao Jangwani
baada ya kusajiliwa msimu huu kwa kuifungia Yanga bao la kwanza dakika
ya 43.
Winga machachari, Simon Msuva akaifungia Yanga bao la pili
dakika ya 45 na Yanga ikaenda kupumzika inaongoza kwa mabao 2-0.
Mzambia mwingine, Obrey Chirwa akaifungia Yanga bao la tatu dakika ya
59, kabla ya Mrundi, Amissi Tambwe kufunga la nne dakika ya 65
na Mzimbabwe Thabani Kamusoko kufunga la tano dakika ya 73.
Ngaya walijipatia bao lao la kufutia machozi dakika ya 66 kupitia kwa
Said Anfane Mohammed aliyetokea benchi kipindi cha pili.
Kikosi cha Ngaya kilikuwa; Said Mmadi, Said Hachim, Said Tothir,
Adhepeau Denis Hubert, Ali Ahmada, Youssouf Ibrahim Moidjie, Zamir
Mohammed, Mounir Moussa, Franck Said Abderemane, Rakoarimanana
Falinurina na Chadhuili Mradabi.
Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Justin Zullu, Simoni Msuva/Emmanuel
Martin, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na
Haruna Niyonzima/Said Juma ‘Maka