Baada ya Jana Feb. 11 Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima kuachiwa na Polisi baada ya mahojiano yaliyodumu kuanzia Alhamisi kituo cha Polisi kati Dar es salaam kufuatia sakata la dawa za kulevya, leo Jumapili February 12 2017 akiwa kwenye Ibada kanisani kwake amesimulia.
‘Nilienda moja kwa moja kwa Kamanda Sirro, nikamkuta na Manji, wakasema wewe na Manji tunakwenda kuwapima kwa mkemia mkuu wa Serikali, wale watu waliokuwa wanapima walikuwa wanapima kwa uwazi kabisa, wakapima vitu vyote majibu hamna chochote’-Askofu Gwajima
“Waliposema twende tukapime nilikua tayari, na mimi nilisema ndani yangu hata ukiona Pombe andika umeona dawa za kulevya, nikasema mimi sina tatizo twendeni nyumbani kwangu na mkikuta hata sigara andikeni ni dawa za kulevya, wakasachi na hawakukuta kitu”