Mwenyekiti wa CCM Mbeya anusurika kuuawa kwa Risasi
Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, Efrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka 60 amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu wasiofahamika.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio
hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 05:45 usiku katika
kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwale, Tarafa ya
Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.
Amesema tukio hilo limetokea wakati akiwa amelala kitandani nyumbani
kwake Ntembela ambapo mbinu iliyotumika ilikuwa ni kukata wavu wa
dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi
za gololi.
Mwenyekiti huyo amefikishwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na hali yake inaendelea vizuri.
Lukula amewaambia waandishi wa habari kuwa nia ya shambulizi hilo
ilikuwa ni kutaka kuumua na kwamba juhudi za kuwatafuta na kuwakamata
wahusika zinaendelea
(Chanzo muungwana blog)