Mwimbaji wa bongofleva Barnaba ambaye ni miongoni mwa waliotoka mbali wakifahamiana na Diamond Platnumz ameyaandika haya kwenye Instagram page yake leo baada ya kuiweka hii picha ya Diamond akiwa na familia yake.
“Ukweli nisiwe muongo kutoka moyoni hii picha inaongea mengi sana nimetazama machozi yamenitoka kabisa kwa furahaa sana, umoja ni nguvu kabisa mkishikana kwa kila matatizo na mkapambana kila kitu kinakua sawa”
“Matatizo ni mengi lakini mwanangu Rafiki Yangu @diamondplatnumz nakupongeza sana kwa kusimama na Familya yako kwa kila mitihani na mbali na mambo Yote ya binadamu na maneno masimango Kash kash za Hapa na pale“