Katika hatua nyingine RC Makonda amekiri kukamatwa kwa Mmiliki wa kituo cha Radio ya EFM,ajulikanae kwa jina la Francis Ciza,almaarufu kwa jina la Dj Majay."tulipokuwa tukifanya opereseheni ya kuwakamata Wahusika wote wa Dawa za kulevya juzi usiku nae akakamatwa kwa mahojiano zaidi; "alisema Makonda.
Makonda amejibu habari za kukamatwa kwa Dj Majay mara baada ya kuulizwa swali na mmoja wa waandishi wa habari, kufuatia tetesi nyingi zilizokuwa zikisambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kukamatwa kwake.