Las Vegas, Marekani
Rene Angelil, mume wa mwanamuziki mashuhuri duniani Celine Dion, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73, nyumbani kwao Las Vegas nchini Marekani baada ya kuugua saratani ya koo iliyomsumbua tangu mwaka 2000.
Bw Angelil alizaliwa mjini Montreal mwaka 1942.
Celine Dion (kushoto) akiwa na wazazi wake pampja na Rene (kulia) mwaka 1982.
Baada ya kuwa meneja wa makundi kadha nchini Canada, aliombwa na wazazi wa Dion awe meneja wake mwanamuziki huyo alipokuwa na umri wa miaka 12 pekee.
Mwaka jana, Dion aliambia gazeti la USA Today kwamba alikuwa akijiandaa kwa kifo cha mumewe.
“Lakini kibarua change kikubwa kitakuwa kumwambia mume wangu kwamba tuko sawa. Nitawatunza na kuwalea watoto wetu. Utatutazama kutoka ulimwengu mwingine.”
Rene amemwachia mjane wake watoto waiwili mapacha Eddy na Nelson (waliobebwa, kwa sasa wana umri wa miaka mitano) na mtoto mwingine mkubwa, Rene Charles Jr. (aliyesimama kulia, kwa sasa ana umri wa miaka 1). Picha zimepigwa mwaka 2011.
Gazeti la Montreal Gazette linasema Bw Angelil aliweka rehani nyumba yake ili kupata pesa za kufadhili albamu ya kwanza ya mwanamuziki huyo.
Mwaka 1999, wimbo wake My Heart Will Go On, uliotumiwa katika filamu ya Titanic, ulishinda tuzo mbili za Grammy.