Rais Magufuli ataka Watanzania waliofungwa nje kwa dawa za kulevya waachwe katika sheria ya Nchi husika




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kuhakikisha vinasimamia sheria ipasavyo ili kukabiliana na tatizo hilo hapa Tanzania.

Ametoa agizo hilo leo tarehe 12 Februari, 2017 Ikulu Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwaapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers William Siyanga, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Joseph Edward Sokoine, Balozi wa Tanzania Algeria Mhe. Omar Yusuf Mzee na Balozi wa Tanzania Uganda Grace Aaron Mgovano.

Hakuishia hapo  Dkt. Magufuli amewataka pia viongozi wote wa Serikali kuungana na vyombo vya dola katika mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na ametaka mapambano hayo yasifanywe kwa mzaha wala kwa kuangalia majina ya watu, vyeo vyao na taasisi wanazoongoza.

Vilevile Rais Magufuli amewapongeza viongozi wote wa mikoa walioanza kukamata watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na amewaomba Watanzania wote waunge mkono juhudi za kukabiliana na wanaofanya biashara na kutumia dawa za kulevya ambazo zinazidi kuangamiza nguvukazi ya Taifa.

“Niwaombe ndugu zangu tuungane katika vita hii dhidi ya dawa za kulevya, waandishi wa habari na wana mitandao tuweke mbele Utanzania wetu, akitokea mtu anapambana na dawa za kulevya tumuunge mkono badala ya kumchafua”
“Vita hii ni kubwa hatuwezi kwenda nayo kwa mzaha na Serikali itahakikisha inasimamia sheria namba 5 ya mwaka 2015 iliyohusu kuzuia na kupambana na dawa za kulevya ambayo ilitungwa na Bunge la 10 lililoongozwa na Spika Anna Makinda na sheria hiyo ikatiwa saini na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, nawapongeza sana kwa kutunga sheria hii.”

Dkt. Magufuli amesema "takwimu zinaonesha kuna watanzania 1,007 wamekamatwa na kufungwa gerezani katika nchi mbalimbali baada ya kupatikana na makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya", na amemuagiza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi hizo kutojihusisha kuwatetea waliofungwa kwa makosa hayo na badala yake waache sheria za nchi husika zichukue mkondo wake bila kujali.

Yanga yaitupia 5-1 Ngaya ya Comoro

 
 
Kikosi cha Yanga kilicho ivuruga Ngaya Leo
YANGA SC wameanza vizuri mawindo yao ya ubingwa wa Afrika, baada ya kwachapa wenyeji Ngaya Club de Mde mabao 5-1 jioni ya leo mjini Moroni, Comoro.
Ushindi huo unamaanisha Yanga watakuwa na shughuli nyepesi tu katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Dar es Salaam, kwani hata wakifungwa 3-0 watasonga mbele.
Kiungo Mzambia, Justin Zulu alifungua akaunti yake ya mabao Jangwani baada ya kusajiliwa msimu huu kwa kuifungia Yanga bao la kwanza dakika ya 43.
 
Winga machachari, Simon Msuva akaifungia Yanga bao la pili dakika ya 45 na Yanga ikaenda kupumzika inaongoza kwa mabao 2-0.
Mzambia mwingine, Obrey Chirwa akaifungia Yanga bao la tatu dakika ya 59, kabla ya Mrundi, Amissi Tambwe kufunga la nne dakika ya 65 na Mzimbabwe Thabani Kamusoko kufunga la tano dakika ya 73.
Ngaya walijipatia bao lao la kufutia machozi dakika ya 66 kupitia kwa Said Anfane  Mohammed aliyetokea benchi kipindi cha pili.
Kikosi cha Ngaya kilikuwa; Said Mmadi, Said Hachim, Said Tothir, Adhepeau Denis Hubert, Ali Ahmada, Youssouf Ibrahim Moidjie, Zamir Mohammed, Mounir Moussa, Franck Said Abderemane, Rakoarimanana Falinurina na Chadhuili Mradabi.
Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Justin Zullu, Simoni Msuva/Emmanuel Martin, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na Haruna Niyonzima/Said Juma ‘Maka

Askofu Gwajima aeleza yaliyotokea POLISI




Baada ya Jana Feb. 11 Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima kuachiwa na Polisi baada ya mahojiano yaliyodumu kuanzia Alhamisi kituo cha Polisi kati Dar es salaam kufuatia sakata la dawa za kulevya, leo Jumapili February 12 2017 akiwa kwenye Ibada kanisani kwake amesimulia.
‘Nilienda moja kwa moja kwa Kamanda Sirro, nikamkuta na Manji, wakasema wewe na Manji tunakwenda kuwapima kwa mkemia mkuu wa Serikali, wale watu waliokuwa wanapima walikuwa wanapima kwa uwazi kabisa, wakapima vitu vyote majibu hamna chochote’-Askofu Gwajima

Waliposema twende tukapime nilikua tayari, na mimi nilisema ndani yangu hata ukiona Pombe andika umeona dawa za kulevya, nikasema mimi sina tatizo twendeni nyumbani kwangu na mkikuta hata sigara andikeni ni dawa za kulevya, wakasachi na hawakukuta kitu”

Wanawake wawili wadakwa na kilo 114 za bangi

Wanawake wawili ni miongoni mwa watu zaidi ya 15 waliokamatwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya.................Published by mwananchi

Kumbe hii ndio Sababu ya Wema Sepetu Kunyimwa Dhamana Wakati Wenzake Wakiondoka Mahakamani kwa dhamana.


Watuhumiwa wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya waliotajwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaamm, Paul Makonda, Jumanne hii, February 7, 2017 wamefikishwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazowakabili.

Mastaa hao wakiwemo TID, Nyandu Tozi, Babu wa Kitaa, Romy Jones, Tunda, na wengine, wameachiwa kwa sharti la dhamana ya shilingi milioni 10 kila mmoja na watakuwa wakiripoti kwa mwezi mara mbili huku wakiwa katika uangalizi wa jeshi la polisi kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Hata hivyo watuhumiwa wengine wakiwemo Petit Man, Said Alteza, Lulu Diva na wengine wametakiwa kuweka dhamana ya shilingi milioni 20 na watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka mitatu. Iwapo watuhumiwa hao watashindwa kufuata masharti hayo watarudishwa tena mahakamani.

Hali hiyo imekuwa tofauti kwa Wema Sepetu ambaye ameendelea kukaa rumande baada ya msako kubaini msokoto wa bangi nyumbani kwake na hivyo kuongezwa kosa jingine zaidi ya lile la awali, ambapo sasa inasubiriwa uchunguzi wake  kukamilika.

Makonda amekiri kukamatwa kwa Mmiliki wa kituo cha Radio ya E-FM



 Katika hatua nyingine RC Makonda amekiri kukamatwa kwa Mmiliki wa kituo cha Radio ya EFM,ajulikanae kwa jina la Francis Ciza,almaarufu kwa jina la Dj Majay."tulipokuwa tukifanya opereseheni ya kuwakamata Wahusika wote wa Dawa za kulevya juzi usiku nae akakamatwa kwa mahojiano zaidi;  "alisema Makonda.
Makonda amejibu habari za kukamatwa kwa Dj Majay mara baada ya kuulizwa swali na mmoja wa waandishi wa habari, kufuatia tetesi nyingi zilizokuwa zikisambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kukamatwa kwake.

Makonda ataja majina mapya 65 ya watuhumiwa dawa za kulevya, Mbowe, Gwajima, Iddi Azan, Manji wamo Ndani ya Dishi

 
Makonda katika picha akiwa na waandishi wa habari
 Akiwa katika awamu ya pili ya kupambana na Biashara ya madawa ya kulevya Makonda ameagiza: Wafuatao (Watu 65) wakutane katika kituo cha kati cha Polisi cha Kanda maalumu ya Dar es salaam Siku ya Ijumaa ambapo miongoni mwao ni, Aikaeli Mbowe (Mbunge wa Hai), Mchungaji Gwajima (Kanisa la Ufufuo na Uzima), Yusuph Manji (M/kiti Yanga), Mmiliki wa Slipway ambae analo eneo la kupaki boti, mmliki wa yatchclub, mmiliki wa MMI, Mwinyi Machata, Rose ambae ana mtandao mpana, Kiboko, Mbunge mstaafu Iddi Azan, Hussein Pamba kali.
 
Kuhusu ishu ya Agness Masogange iliyosemwa na Wema Sepetu? Paul Makonda amejibu hivi:

"Mimi nina kifua cha kuhimili mikiki yote, kwa hiyo ni kama ina niongezea nguvu, sasa wewe umekamatwa unashindwaje kumtaja muhusika akakamatwa na uko sehemu husika? Hata hivyo mtu ukiwa mahabusu unawezaje kutumia simu? Hilo ni kosa na sasa vyombo vya usalama vina lishughulikia hilo"
‘Haya mengine yanaoendelea kama mtu ana ushahidi anatupa taarifa tumekamata  watu zaidi 120 kupitia taarifa tulizozipata sasa wewe umeshindwaje kumtaja naye akafuatwa’

Askofu Gwajima Amjibu Makonda kwa Ujumbe Huu wa picha


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Katika picha akiongea na waandishi


Saa chache baada ya Askofu Gwajima kutakiwa kufika polisi na mkuu wa mkoa kwa kutoa taarifa juu ya madawa ya kulevya,Askofu Gwajima Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Amepost Ujumbe picha huu ambao wadadisi wa mambo wanadai kuwa ni kama jibu kwa Mhe Makonda.



Askofu Mkuu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima

Makonda, TID waonekana pamoja Instagram


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akiwa na msanii wa Bongo fleva Khalid mohamed (TID)
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameonekana kwenye ukurasa wake mtandao wa instagram akiwa na msanii Khalid Mohamed ‘TID’ ambaye siku chache zilizopita alimtaja katika orodha ya watuhumiwa wa kujihusisha na dawa za kulevya.

Baada ya kutajwa, TID akiwa na wasanii kadhaa waliotajwa na mkuu huyo wa mkoa walifika Kituo Kikuu cha Polisi jijini humo na kuhojiwa kisha kuachiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lakini ikiwa ni baada ya kuwekwa chini ya uangalizi wa mwaka mmoja.

Kuonekana kwa Makonda akiwa na TID kumeibua mijadala kuwa huenda ameanza kukutana na watu aliowataja kutumia dawa za kulevya ili kutatua tatizo hilo.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Makonda ameweka picha inayomuonyesha akiwa na msanii huyo.

Pamoja na picha hiyo, Makonda ameandika “Mungu wetu hajalala na siku zote anampenda amtafutae, karibu tena nyumbani TID”.

Picha hiyo pia inaonekana kwenye ukurasa wa instagram wa TID ikiwa na maneno “muziki bila dawa za kulevya inawezekana....This is the turning point kwangu mimi na kizazi cha muziki huu wa kizazi kipya, nikiwa na Mh. Makonda leo tukijadili jinsi ya kuokoa vipaji na sanaa kwa ujumla, Mungu ibariki Bongo fleva, Mungu ibariki Tanzania”. Amen  Makonda na TID Mungu kweli anatuona.